Wednesday, 25 February 2015

KILIO CHA HAKI

Mioyo yetu yaumia, ndoto zetu za didimia,
Wakati wetu wa timia, duniani twapitia,
Swali langu kwa wakenya, mbona chuki kwa wenzetu?

Usalama wa mwananchi, ni hekaya kwa Abunuasi
Ukijiburudisha kilabuni, kuamka kesho jinamizi
Swali langu kwa wakenya, atakeyekufa kesho ni nani?

Twapoteza wahitajika, kwa vinyweo kadhalika
kwani kifo hakina huruma, kwa mkenya mheshimiwa
dua langu kwake Mola, laza roho zetu pahali pema.



No comments:

Post a Comment